DAWA NA TIBA
Faida za Kiafya za Kitunguu Swaumu (Garlic)
Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.
Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen'genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.
Historia inaonesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika China mwaka 510 K.K na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Roma. Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana.
Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza kutumika kama dawa ya kusafishia vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza na pili ya dunia. Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa kwa kutumia jamii hii ya vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo (mouth wash) ingawa watumaiji wake wengi huilalamikia dawa hiyo kwa sababu ya harufu mbaya ya dawa hiyo inayowasababishia kunuka kwa mdomo.
Faida za vitunguu swaumu
Katika tafiti mbalimbali vitunguu swaumu vimeonekana kuwa na uwezo wa kutibu maambukizi ya bakteria, fangasi na virusi vya aina mbalimbali. Aidha husaidia kuzuia magonjwa ya moyo ikiwemo kuondoa lijamu katika mishipa ya damu na hivyo kusaidia katika kurekebisha shinikizo la damu. Faida nyingine za vitunguu swaumu ni pamoja na
Katika utafiti uliofanyika nchini Czech ilionekana kuwa matumizi ya vitunguu swaumu yalisaidia sana katika kupunguza kusanyiko la lijamu (cholesterol) pamoja na mafuta yasiyofaa mwilini (low density lipoproteins) katika mishipa ya damu. Aidha, mwaka 2007 BBC iliripoti matumizi ya vitunguu swaumu katika kusaidia kumkinga mtumiaji dhidi ya aina fulani ya mafua iliyosababishwa na virusi. Mwaka 2010, ulifanyika utafiti mwingine ambao ulijumuisha wagonjwa 50 wenye shinikizo la damu sugu ambalo lilikuwa ni vigumu kudhibitiwa hata kwa matibabu yaliyozoeleka ya dawa na njia nyingine. Kama njia ya kuchunguza ufanisi wa vitunguu swaumu katika kutibu shinikizo la damu, baadhi ya wagonjwa hao walipewa vitunguu swaumu wakati wengine walipewa dawa isiyohusika na matibabu ya shinikizo la damu (au placebo). Ilionekana kuwa wale waliopewa vitunguu swaumu kama dawa ya shinikizo la damu walionesha maendeleo mazuri kwa vitunguu swaumu kuweza kushusha vizuri kiwango cha shinikizo la damu, hususani systolic pressure, tofauti na wale waliopewa placebo.
Nini siri ya kitunguu swaumu?
Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;
Ukiacha faida zake, vitunguu swaumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na;

- Kutibu saratani ikiwemo saratani ya tumbo na utumbo mkubwa. Tafiti zinaonesha idadi ndogo ya wagonjwa wa saratani katika nchi ambazo wakazi wake wana utamaduni wa kutumia vitunguu swaumu kwa wingi.
- Vitunguu swaumu husaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu. Hata hivyo inashauriwa kwamba wagonjwa wa kisukari wanaotumia sindano za insulin wasitumie kitunguu swaumu kwa wingi mpaka watakaposhauriwa na daktari.
- Huzuia kusanyiko la chembe sahani zinazosaidia kuganda kwa damu (platelet aggregation)
- Husaidia ufyozwaji wa thiamin, hivyo kusaidia kuepusha mwili na ugonjwa wa beriberi
- Ina kiasi kikubwa cha vitamini C ambayo husaidia kuzuia ugonjwa wa kiseyeye
- Hutumika kutibu magonjwa nyemelezi kama toxoplasmosis, hasa kwa watu wenye upungufu wa kinga mwilini.
Katika utafiti uliofanyika nchini Czech ilionekana kuwa matumizi ya vitunguu swaumu yalisaidia sana katika kupunguza kusanyiko la lijamu (cholesterol) pamoja na mafuta yasiyofaa mwilini (low density lipoproteins) katika mishipa ya damu. Aidha, mwaka 2007 BBC iliripoti matumizi ya vitunguu swaumu katika kusaidia kumkinga mtumiaji dhidi ya aina fulani ya mafua iliyosababishwa na virusi. Mwaka 2010, ulifanyika utafiti mwingine ambao ulijumuisha wagonjwa 50 wenye shinikizo la damu sugu ambalo lilikuwa ni vigumu kudhibitiwa hata kwa matibabu yaliyozoeleka ya dawa na njia nyingine. Kama njia ya kuchunguza ufanisi wa vitunguu swaumu katika kutibu shinikizo la damu, baadhi ya wagonjwa hao walipewa vitunguu swaumu wakati wengine walipewa dawa isiyohusika na matibabu ya shinikizo la damu (au placebo). Ilionekana kuwa wale waliopewa vitunguu swaumu kama dawa ya shinikizo la damu walionesha maendeleo mazuri kwa vitunguu swaumu kuweza kushusha vizuri kiwango cha shinikizo la damu, hususani systolic pressure, tofauti na wale waliopewa placebo.
Nini siri ya kitunguu swaumu?
Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;
- Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
- Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
- Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
- Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo inayotolewa baada ya kuvila.
Ukiacha faida zake, vitunguu swaumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na;
- Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa au kunywa maji mengi.
- Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)
- Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha.
- Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.
- Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.
- Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.
DAWA ZA KULEVYA NA ATHARI ZAKE
Tatizo la madawa ya kulevya limetokea kuwa janga kubwa duniani kote, watu wengi wameathirika na janga hili. jinsia zote wanaume, wanawake, na vilevile rika zote vijana na wazee pia. Hapa tutaongelea aina mbili za madawa ya kulevya yaani Cocaine na Heroin.
Cocaine
Hutokana na majani ya mmea uitwao kitaalamu Erythroxylum coca bush.
Aina hii ya dawa ya kulevya hutolewa kwa mifumo ifuatayo;
Mara tu baada kutumia dawa hii dalili zifuatazo hutokea
Baada ya kutumia cocaine kwa muda mrefu punde unapoacha tu kutumia dalili zifuatazo hutokea;
Hujulikana vilevile kama diamorphine, hutokana na mmea huitwao kitaalamu opium poppy. Heroin kwa mfumo wa Morphine hutumiwa hospitalini kama dawa ya maumivu makali ya ghafla (acute pain) kwenye maumivu makali ya kifua wakati wa shambulizi la moyo, na kwa maumivu ya mtu aliyepata ajali, vilevile baada ya upasuaji, na maumivu sugu kwenye kansa. Hivyo hutolewa kwa kuangalifu mkubwa.
Aina hii ya dawa ya kulevya huweza kutumika kwa kuvuta kwa pua, kuvuta kama sigara na kwa kuchoma kwenye mshipa. Siku hizi watu hutumia njia ya haja kubwa na kwenye uke, ambapo kuta hufyonza heroin na kuanza kufanya kazi ndani ya sekunde arobaini.
Heroin mara tu baada ya kuingia kwenye damu kuenda kwenye mfumo wa neva na kukandamiza ufanyaji kazi wake, ndio huweza kutumika kupunguza maumivu.
Dalili za mtu aliyetumia heroin
Dalili ambazo hutokea mara tu anapotumia Heroin:
Madhara ya matumizi ya muda mrefu wa dawa hii ya kulevya hutokana zaidi na matumizi ya sindano na vifaa vingine visivyo salama

- Unga ambapo mitaani hujulikana kama ‘coke’ na hutumika kwa kuvutwa puani kama unga, au kuyeyushwa na maji na kuchomwa kwenye mshipa wa damu.
- Crack ambapo mitaani hujulikana kwa jina hilohilo crack au rock, na hutengenezwa kwa kuchanganywa na kemikali. Na hutumika kwa kuvutwa kama sigara.
Mara tu baada kutumia dawa hii dalili zifuatazo hutokea
- Mishipa ya damu husinyaa (constricted blood vessels)
- Joto la mwili huongezeka
- Mapigo ya moyo huongezeka
- Shinikizo la damu
- Dilated pupils
- Moyo - Kwenye moyo huweza kuleta Shambulizi la moyo (heart attack) na vilevile mapigo ya moyo yasiyo na mpangilio (Arrhythmia) hivyo unaweza kufa ghafla tu.
- Ubongo - Mishipa ya damu kwenye ubongo inaweza kusinyaa na kupelekea kupata Kiharusi, hata kwa kijana. Vilevile unaweza kupata ugonjwa wa akili (substance abuse pyschosis).
- Mapafu na mfumo wa hewa - Uvutaji kupitia pua huweza kupelekea tatizo sugu la kutokwa damu puani kila wakati na mafua yasiyo pona, kupoteza mfumo wa harufu, na ikivutwa kama sigara kuharibu mapafu moja kwa moja.
- Mfumo wa chakula - Cocaine husababisha kusinyaa kwa mishipa ya damu kwenye tumbo na utumbo hivyo kusababisha vidonda na kuweza kuharibu kabisa mfumo huu kwa utumbo kuoza.
- Mafigo - kutokana na shinikizo la damu mafigo yanaweza kushindwa kufanya kazi vizuri, vilevile cocaine inaweza kuleta madahara moja kwa moja kwenye mafigo kitaalamu Rhabdomyolysis.
- Ngono - ingawa cocaine huweza kutumika kama njia ya kuongeza hamu ya ngono huweza kusababisha kushindwa kumaliza kile ulichokianza. Matumizi sugu ya dawa hii ya kulevya huleta madhara kwa jinsia zote yani kwa wanaume na wanawake.
- Na vilevile huweza kufanya kuwa tegemezi wa dawa hii.
- Kwa wanaotumia sindano na kushea wanaweza kupata maambukizi ya virusi ya hepatitis na vya ukimwi.
Baada ya kutumia cocaine kwa muda mrefu punde unapoacha tu kutumia dalili zifuatazo hutokea;
- Unyogovu
- Uchovu
- Kushindwa kuzingatia na kutokuwa makini
- Kukosa uwezo wa kuwa na furaha au kusikia raha
- Kuongezeka kwa tama zaidi ya kutumia cocaine
- Kujisikia kuumwa, maumivu, baridi na kutetemeka.
- Moyo kushindwa kufanya kazi
- Kiharusi
- Degedege mara kwa mara
- Mfumo wa hewa kushindwa kufanya kazi
Hujulikana vilevile kama diamorphine, hutokana na mmea huitwao kitaalamu opium poppy. Heroin kwa mfumo wa Morphine hutumiwa hospitalini kama dawa ya maumivu makali ya ghafla (acute pain) kwenye maumivu makali ya kifua wakati wa shambulizi la moyo, na kwa maumivu ya mtu aliyepata ajali, vilevile baada ya upasuaji, na maumivu sugu kwenye kansa. Hivyo hutolewa kwa kuangalifu mkubwa.
Aina hii ya dawa ya kulevya huweza kutumika kwa kuvuta kwa pua, kuvuta kama sigara na kwa kuchoma kwenye mshipa. Siku hizi watu hutumia njia ya haja kubwa na kwenye uke, ambapo kuta hufyonza heroin na kuanza kufanya kazi ndani ya sekunde arobaini.
Heroin mara tu baada ya kuingia kwenye damu kuenda kwenye mfumo wa neva na kukandamiza ufanyaji kazi wake, ndio huweza kutumika kupunguza maumivu.
Dalili za mtu aliyetumia heroin
Dalili ambazo hutokea mara tu anapotumia Heroin:
- Kujisikia mwenye furaha na raha
- Kupishana Kusikia hali usingizi na tahadhari
- Midomo kuwa mikavu
- Misuli kuishiwa nguvu
- Kuhema polepole
- Warm skin flushing
- Mikono na miguu kuwa mizito
- kope za macho kulegea
Madhara ya matumizi ya muda mrefu wa dawa hii ya kulevya hutokana zaidi na matumizi ya sindano na vifaa vingine visivyo salama
- Maambukizi kwenye kuta na milango ya moyo
- Maambukizi ya ini na virusi (kama hepatitis C na HIV),
- Maambukizi ya figo
- Maambukizi ya mfumo wa hewa
- Maambukizi ya ngozi na majipu
- Kutotulia
- Maumivu ya misuli na mifupa
- Kutapika
- Dalili hizi hufikia kilele ndani ya masaa 48 hadi 72 na hufika kikomo baada ya wiki.